ANNOUNCEMENT One Day International Apostolic Conference: Location: KIA (Mianzini) on 20th October 2026 Contact: 0692937637/0754757658
IMANI NI NINI?

IMANI NI NINI?

Text Size: 100%
PDF
Soma kwa Sauti:
Reading...

IMANI NI NINI?

       1. Imani ni ushawishi unaotokana na kusikia. WARUMI 10:17,
        2. Inaambatana na kutumaini na kuamini.

KATIKA BIBLIA Neno "Imani" linatumika likiongea habari za MUNGU au YESU KRISTO au mambo ya kiroho.

Tunapoona na kutambua dhambi zetu tunapatwa na hofu ya kiungu na kutubu. Lakini tusipoamini kuwa tumesamehewa dhambi zetu, toba yetu ni bure.

Mtu anapotambua yeye ni mwenye dhambi, akitubu ni lazima aamini kuwa amesamehewa dhambi zote, hapaswi kufikiria tena dhambi alizozitenda zamani. ISAYA 1:18,

Tusipoamini kwamba YESU ameziondoa dhambi zetu, hukumu na aibu bado itakuwa ndani mwetu na itasababisha toba yetu kuwa bure.

      Kutubu ni kugeuka na kuachana na Dhambi, na kuwa na IMANI na kumgeukia MUNGU wa Kweli.

Kwa IMANI:

  = Tunampokea YESU KRISTO haswa kama alivyo ktk injili.

  = Tunamtumaini na kujikabidhi kwake jumla.

  = Tunakubaliana na ahadi za MUNGU kwetu kupitia YESU.

Biblia inasemaje ju ya IMANI?

Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo ya yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasioonekana" EBRANIA 11:1.
Yatarajiwayo na yasioonekana yanakuwa hakika kwa maana tunamtumaini MUNGU.

Kama tulivyoona kuwa imani ni ushawishi unaotokana na kusikia.

. Tunaamini kwamba  MUNGU anaweka ahadi zake kwa waaminio.

Lakini BWANA ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu. 2THESALONIKE 3:3,
. Tunaamini kwamba MUNGU anaweza kutenda yale aliyoahidi atatenda " 
Huku akijua hakika ya kuwa MUNGU aweza kufanya yale aliyoahidi, WARUMI 4:21,

Mtu hawezi kuokolewa pasipo IMANI.

   1: Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiye amini, atahukumiwa" MARKO 16:16, 
Zingatia hapa, tambua anaesikia na kuamini na kubatizwa  ni Mtu mzima, (siyo mtoto)

   2: Wokovu ni kipawa kinachopokelewa kwa IMANI. 
Kwa Maana mmeokolewa kwa Neema, Kwa njia ya Imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU" WAEFESO 2:8,

Mtu hawezi kumpendeza MUNGU pasipo IMANI.

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; EBRANIA 11:6, 
IMANI ziko nyingi sana, ila imani ya Kweli inapatilana kwa YESU tu.

Maana hii imani Siyo ya dini, ni imani ndani ya KRISTO YESU, ukiamini unakuwa wa YESU, wengi wameamini dini zao, Siyo vibaya kuamini dini yako,  ila tambua dini siyo MUNGU, na MUNGU hana dini yake,
MUNGU ana Watu walioamini, ndo wanaitwa Wakristo, maana wana ROHO wa MUNGU ndani yao.

Tunapokeaje Imani? Basi Imani, chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa NENO la KRISTO, 
WARUMI 10:17,

NENO la MUNGU ni yale MUNGU anasema, hivyo ni, BIBLIA inatakiwa kusomwa na kuamini kama ilivyoandikwa.

MUNGU anaendelea kusema nasi kupitia Mwana, ambaye ni NENO linaloishi. EBRANIA 1:2, YOHANA 1:1, 
Na YESU alisema; 
Mtu hataishi kwa Mkate tu, ila kwa kila NENO litokalo ktk kinywa cha MUNGU. MATHAYO 4:4,

1. Tunamsikia MUNGU akisema nasi binafsi tunaposoma BIBLIA. 
2. Tunapokea IMANI ya kufanya yale tumesikia. 
3. YESU anakuwa hakika kwetu. Yeye ni NENO alifanyika mwili. YOHANA 1:14,

Kujua habari za MUNGU tu hakukuakikishii wokovu, 
Wewe waamini ya kuwa MUNGU ni mmoja; watenda vema; mashetani nao waamini ma kutetemeka. 
YAKOBO 2:19,

SHALOM. Nitaendelea.

Maoni & Tafakari za Wasomaji (0)

Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!

Acha Tafakari Yako
NENO TIME
Sakinisha App ya NENO TIME
Upatikanaji wa haraka na masomo bila intaneti