ANNOUNCEMENT One Day International Apostolic Conference: Location: KIA (Mianzini) on 20th October 2026 Contact: 0692937637/0754757658
IBRAHIMU - BABA WA WOTE WANAOAMINI.

IBRAHIMU - BABA WA WOTE WANAOAMINI.

Text Size: 100%
PDF
Soma kwa Sauti:
Reading...

IMANI ni:
   1. Maamzi ya kupokea          NENO tulilolisikia. 
   2. Kupokea kwa kumwamini yule ambaye amelinena ktk mioyo yetu.
   3. Kumgeukia MUNGU na kubadilila tunapomtumaini atimize NENO lake.
   4. Kudhawabiwa kwa kutambua ya kuwa MUNGU ni Mwaminifu na anaweka ahadi zake.

IBRAHIMU - BABA WA WOTE WANAOAMINI.

Katika WARUMI 4:3, Paulo anaonyesha kutembea kwa IMANI kwa mfano wa Ibrahimu;

= MUNGU alimhesabu Ibrahimu kama Mtu mwenye haki kwa sababu alimwamini MUNGU. (Mst 3)

= Ibrahimu alisikia na kupokea NENO kutoka kwa MUNGU,  WARUMI 4:13, 21,

= Ibrahimu aligeuka kwa IMANI kutoka kwa hali yake isiyokuwa na matumaini, WARUMI 4:18-20,

= Ibrahimu aliamini na akashikilia ahadi ambayo  MUNGU alimpa ktk, Mwazo 15:3-6, (18)

= Ibrahimu hakusita kwa kutokuamini, WARUMI 4:20,
= Ibrahimu alitiwa nguvu kwa IMANI, akimtukuza MUNGU mst 20,

Hapa tunamwona Ibrahimu akiamini kile ambacho hajakiona, je wewe unaamini unachokiona au usichokiona?

Tambua IMANI ni hakika, na ni bayana. 
WAEBRANIA 11:1, 2Korintho 4:18,

WAEBRANIA 11:8-9,

= Kwa IMANI Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako, 
= Kwa IMANI alikaa ugenini ktk ile nchi ya ahadi. 

- Hebu tufikiri kwa pamoja, je unaamini nini!

Je IMANI yako iko ktk vitu ulivyonavyo au kwa nani? Je ulichokiwekea IMANI au kukitumainia kikiondoka utakuwa salama ktk Maisha yako!  Jiulize. YEREMIA 17:5-6,

SHALOM: Tunaendelea na somo letu la IMANI.

Leo hebu tuwatazame watu waliosimama imara ktk IMANI.

EBRANIA 11 Unatuambia kuhusu watu wengine wa IMANI. Hawa wote walikufa ktk IMANI, bila kuipokea ahadi, lakini wakiziona kwa mbali, walihakikishiwa, wakazikumbatia na wakakiri kuwa walikuwa wageni na wapitaji hapa duniani, EBRANIA 11:13,

Na watu wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya Imani yao, hawakuipokea ahadi, Kwa kuwa MUNGU alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisI. EBRANIA 11:39-40,

Unaona hiyo!  Yaajabu sana!

YESU NDIYE UTIMILIFU WA" kitu kilicho bora.

Wakati YESU alianza huduma yake na kufanya muujiza ktk harusi ya kana, tunasoma kwamba" wanafunzi wake walimwamini. YOHANA 2:11,

Makutano walimuuliza YESU watafanya ili kuzitenda kazi za MUNGU?  YESU aliwajibu;  hii ndiyo kazi ya MUNGU, nimwamini Yeye aliyetumwa na Yeye. YOHANA 6:29,

USIWE MTU WA KUONA NA KUAMINI, NA USIWE MTU WA KUTUMAINI UNACHOKIONA, (Bali kuwa Mtu wa IMANI)

= YESU akamwambia, umeamini kwa kuwa Umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini, YOHANA 20:29,
= YESU akageuka, naye alipomwona akamwambia, Binti, jipe moyo mkuu, IMANI yako imekuponya. MATHAYO 9:22,

YESU anahitaji watu wanaoamini pasipo kuona chochote, usijaribu kuweka sanamu ya namna yoyote ukaifananisha na MUNGU, KUMBU LA TORATI 4:15-19, ISAYA 46:1-2, inasema Vinyago pamoja na wale wanaovibeba vinainama chini. 
Hiyo miungu haiwezi kuwaokoa watu.

= Vipofu wawili walimwani YESU wakaponywa MATHAYO 9:29,
= Akida (jemadari) pia alimwamini YESU na Mtumishi wake akapona. MATHAYO 8:13,

Hawa wote waliweka IMANI kwa MUNGU na mjibu yakatokea.

Je wewe ndg IMANI yako umeiweka wapi? Je ni kwenye sanamu! Fedha, mali, watoto, wazazi, nk, tafakari chua hatua.

SHALOM Nitaendelea

Maoni & Tafakari za Wasomaji (0)

Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!

Acha Tafakari Yako
NENO TIME
Sakinisha App ya NENO TIME
Upatikanaji wa haraka na masomo bila intaneti