ANNOUNCEMENT One Day International Apostolic Conference: Location: KIA (Mianzini) on 20th October 2026 Contact: 0692937637/0754757658
Hebu tumtazame Paulo anachokizungumza kuhusu IMANI.

Hebu tumtazame Paulo anachokizungumza kuhusu IMANI.

Text Size: 100%
PDF
Soma kwa Sauti:
Reading...

Hebu tumtazame Paulo anachokizungumza kuhusu IMANI.

1. Ili IMANI yenu isiwe ktk  hekima ya wanadamu, bali ktk nguvu za MUNGU, 1KORINTHO 2:5,
2. Na kama KRISTO hakufufuka, IMANI yenu ni bure; mngalimo ktk dhambi zenu, 1KORINTHO 15:17,
3. Kwa IMANI yenu mnasimama 2Korintho 1:24,

Tambua Mtu aliye amini IMANI yake iko ndani ya YESU KRISTO aliyefufuka, 1KORINTHO 15:20,

Hebu tumtazame tena YAKOBO ndg yake YESU.

Ila aombe kwa IMANI, pasipo shaka yo yote, YAKOBO 1:6.

Kwa IMANI ndani ya YESU KRISTO tunapokea.

= Ahadi ya ROHO Mtakatifu. Wagalatia 3:14,
= Tunapokea uwana GALATIA 3:26,
=  Wokovu EFESSO 2:8 
= Kumfikia Baba EFESSO 3:11-12,

Kwa IMANI ndani ya YESU KRISTO 
1. Tumefanyika haki WARUMI 5:1a.
2. Tuna amani na MUNGU WARUMI 5:1b.
3. Tumeifikia Neema ya MUNGU. WARUMI 5:2a
4. Tunafurahia ktk tumaini la utukufu wa MUNGU. WARUMI 5:2b.

Mara tunapoweka Msingi wa kutubu na kubatizwa na kumpokea ROHO Mtakatifu  ktk Maisha yetu, tunafanywa haki na MUNGU kwa kuamini kwetu. MUNGU anahitaji tuishi kama Ibrahimu alivyoishi.
Huku akijua hakika ya kuwa MUNGU aweza kufanya yale aliyoahidi. 
WARUMI 4:21,

Ukweli wa imani yetu unaweza kujaribiwa, lakini tukibaki waaminifu,  

Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, Kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, ktk kuupokea mwisho wa IMANI yetu, yaani, wokovu wa roho zenu. 
1PETRO 1:8-9,

Ndg IMANI yetu inajengwa ndani ya YESU KRISTO tu. Tambua IMANI ya kweli haiko kwenye dini au madhehebu  yalioanzishwa na wanadamu,

IMANI ya kweli ya waliomwamini YESU na hawana ubinafsi wa dini. Bali ni wamoja ktk mwili wa KRISTO. YOHANA 17:20-23,

IMANI ya kweli kwa waliomwamini YESU, hawagawanywi na dini au madhehebu. 1KORINTHO 1:10-13, 
Tafakari sana chukua hatu hizi ni nyakati za mwisho, YESU haji kuchukua watu wa dini au wa madhehebu, anakuja kwa Kanisa lake analoliandaa.

SHALOM: nimemaliza somo letu la Msingi wa imani, tarajia somo jingine,

Maoni & Tafakari za Wasomaji (0)

Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!

Acha Tafakari Yako
NENO TIME
Sakinisha App ya NENO TIME
Upatikanaji wa haraka na masomo bila intaneti