ANNOUNCEMENT One Day International Apostolic Conference: Location: KIA (Mianzini) on 20th October 2026 Contact: 0692937637/0754757658
Ukurasa wa Maombi

Simameni Pamoja Katika Maombi

"Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii." — Yakobo 5:16

Ukurasa wa Maombi
4
Jumla ya Maombi
13
Maombi Yaliyotolewa
Ndugu / Dada katika Kristo
Tanzania • Sep 29, 2026
Kuombea kujifungua salama

Habari wapendwa Ninaomba mniombee/mniweke kwenye maombi natarajia kujifungua hivi karibuni maombi yenu yanaitajika Mungu awabariki sana

Mama allan
Tanzania • Sep 29, 2026
Kuombea ndoa yangu inachangamoto za mipango yakando

Mnisaidie kuomba wapendwa

Mwamini Asiyejitambulisha
Tanzania • Sep 29, 2026
KUMUOMBEA MGONJWA NDUGU PROSPER NCHIMBI

Shalom shalom wapendwa katika Bwana! Naomba tumuombee huyu ndugu PROSPER NCHIMBI anasumbuliwa na ugonjwa wa Tenzi dume pamoja na Figo ! Kila mtu kwa Imani yake naomba tumuombee ili aweze kurudi kwenye Hali yake! Maana ameshapelekwa sana hospital mpaka kufika hapa madaktari wameshindwa na wamemrudiaha nyumbani. Ila naamini kwa Mungu hakuna jambo lisiloshindikana! Mbarikiwe sana

Mwamini Asiyejitambulisha
Tanzania • Sep 28, 2026
Mama Mgonjwa

Habari za uzima wapendwa. Tafadhali niungeni mkono mimi na familia yangu katika maombi yenu wiki hii. Mama yangu amekuwa akiugua kwa wiki mbili sasa, akisumbuliwa na uchovu uliokithiri pamoja na homa kesho anaenda kufanyiwa vipimo muhimu vya kimatibabu katika hospitali hapa Arusha. Mungu awabariki sana kwa kutukumbuka mioyoni mwenu na katika maombi yenu.

Jinsi Maombi Yanavyofanya Kazi
  • Shiriki Mzigo Wako: Wasilisha ombi la maombi kwa ajili yako, familia, kuponywa, au mwongozo wa kiroho.
  • Waombee Wengine: Bofya "Nimeombea Hili 🙏" kwenye ombi lolote ili kumjulisha mwombaji kuwa umemwombea.
  • Baki Bila Kutaja Jina (Hiyari): Unaweza kuchagua kuchapisha bila kutaja jina au kushiriki jina lako na nchi.
NENO TIME
Sakinisha App ya NENO TIME
Upatikanaji wa haraka na masomo bila intaneti