Habari wapendwa Ninaomba mniombee/mniweke kwenye maombi natarajia kujifungua hivi karibuni maombi yenu yanaitajika Mungu awabariki sana
Mnisaidie kuomba wapendwa
Shalom shalom wapendwa katika Bwana! Naomba tumuombee huyu ndugu PROSPER NCHIMBI anasumbuliwa na ugonjwa wa Tenzi dume pamoja na Figo ! Kila mtu kwa Imani yake naomba tumuombee ili aweze kurudi kwenye Hali yake! Maana ameshapelekwa sana hospital mpaka kufika hapa madaktari wameshindwa na wamemrudiaha nyumbani. Ila naamini kwa Mungu hakuna jambo lisiloshindikana! Mbarikiwe sana
Habari za uzima wapendwa. Tafadhali niungeni mkono mimi na familia yangu katika maombi yenu wiki hii. Mama yangu amekuwa akiugua kwa wiki mbili sasa, akisumbuliwa na uchovu uliokithiri pamoja na homa kesho anaenda kufanyiwa vipimo muhimu vya kimatibabu katika hospitali hapa Arusha. Mungu awabariki sana kwa kutukumbuka mioyoni mwenu na katika maombi yenu.