ANNOUNCEMENT One Day International Apostolic Conference: Location: KIA (Mianzini) on 20th October 2026 Contact: 0692937637/0754757658
YESU ALIKAMATWA

YESU ALIKAMATWA

Text Size: 100%
PDF
Soma kwa Sauti:
Reading...

Alikamatwa na watu wengi waliokuwa na rungu na
panga. Mmoja wa wanafunzi Wake alijaribu kumtetea,
kwa kukata sikio la mmoja wa watu hao.
“Basi alipokuwa akinena bado, tazama, Yuda, mmoja
wa wale kumi na wawili, akaja pamoja na kundi kubwa
lenye panga na rungu, kutoka kwa wakuu wa makuhani
na wazee wa watu… Na ghafula, mmoja wa wale
waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake,
akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa
kuhani mkuu, akalikata sikio lake.” Mathayo 26:47, 51
Yesu alimponya yule mtu ambaye sikio lake lilikatwa!
Hakuogopa kwa ajili ya maisha yake bali hata
aliwaza kuwasaidia maadui zake! Naye Yesu
alimkemea mwanafunzi wake kwa tendo hilo.
“Akagusa sikio lake, akamponya.” Luka 22:51
“Lakini Yesu akamwambia, ‘Rudisha upanga wako
mahali pake; kwa maana wote wautumiao upanga
watakufa kwa upanga.’” Mathayo 26:52
Kisha Yesu alieleza kuwa angeweza kuita malaika
wengi ili wamsaidie kama angetaka, lakini jambo
la muhimu zaidi lilikuwa kuendelea na mpango wa Mungu.
“Je, unadhani ya kuwa siwezi kumwomba Baba yangu,
naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na
mawili ya malaika? Basi Maandiko yatatimiaje,
ya kwamba lazima iwe hivi?” Mathayo 26:53-54
Wanafunzi walimwacha
“Ndipo wanafunzi wake wote walipomwacha
wakakimbia.” Mathayo 26:56
YESU ALISHITAKIWA KWA UONGO
Viongozi wa watu walitafuta sababu za
kumwua. “Basi wakuu wa makuhani, wazee na baraza walitafuta
ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu ili wamuue…”
Mathayo 26:59
Alipelekwa mbele ya Kuhani Mkuu (kiongozi mkuu
wa kidini wa wakati huo) na mashahidi wa uongo
wakatoa ushahidi dhidi ya Yesu. Yesu alikaa kimya
na hakujibu maswali yao.
“Lakini hatimaye mashahidi wawili wa uongo walijitokeza na kusema,
‘Mtu huyu alisema, ‘Ninaweza kulivunja hekalu la Mungu
na kulijenga upya kwa siku tatu.’’ Kisha kuhani mkuu akasimama
na kumwambia, ‘Je, hujibu lolote? Ni nini
hicho ambacho watu hawa wanashuhudia dhidi yako?’ Lakini Yesu alikaa
kimya.” Mathayo 26:60-63

Maoni & Tafakari za Wasomaji (0)

Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!

Acha Tafakari Yako
NENO TIME
Sakinisha App ya NENO TIME
Upatikanaji wa haraka na masomo bila intaneti