ANNOUNCEMENT One Day International Apostolic Conference: Location: KIA (Mianzini) on 20th October 2026 Contact: 0692937637/0754757658
YESU ALIJIONYESHA KWA WENGI

YESU ALIJIONYESHA KWA WENGI

Text Size: 100%
PDF
Soma kwa Sauti:
Reading...

Yesu alifufuka kutoka kwa wafu na akaonekana na watu
wengi. Katika tukio moja, alionekana na watu wapatao
500 kwa wakati mmoja!
“…na ya kuwa alifufuka siku ya tatu kama Maandiko
yasemavyo, na ya kuwa alionekana na Kefa (Petro), kisha
na wale kumi na wawili. Baada ya hayo alionekana na ndugu
zaidi ya mia tano kwa wakati mmoja, ambao wengi wao
bado wako hai hata sasa, lakini wengine wamelala mauti.
Baada ya hayo alionekana na Yakobo, kisha na mitume
wote. Mwisho kabisa alionekana na mimi pia (Paulo)…” 1 Wakorintho
15:4-8
YESU ALIFUFULIWA KUTOKA KWA WAFU ILI
ATUFANYE KUWA WENYE HAKI KAMA VILE
HATUKUWAHI KUTENDA DHAMBI! ILI
ATUPE UHAI MPYA!
Alifufuliwa kwa ajili ya kuhesabiwa haki kwetu [kutufanya
huru kutoka dhambini na kuishi maisha mapya].
“Alitiwa mikononi mwa watu kwa ajili ya makosa yetu,
akafufuliwa kwa ajili ya kuhesabiwa haki kwetu.” Warumi 4:25
Kwa kuamini na kubabatizwa katika jina la Yesu,
tunapokea uhai na nguvu ileile iliyomfufua
Yesu kutoka kwa wafu! Tunaishi kwa uhai Wake!
“Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika
mauti, ili kama Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa
utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika
upya wa maisha!” Warumi 6:4
YESU YU HAI LEO!
YUKO WAPI SASA?
Yesu ameketi mkono wa kuume wa Mungu mbinguni.
Hii ni nafasi ya mamlaka kamili juu ya vitu
vyote mbinguni na duniani!
“Basi, baada ya Bwana kusema nao, alichukuliwa juu
mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.” Marko 16:19
“…kwa kadiri ya utendaji wa nguvu zake kuu ambazo
alizitenda ndani ya Kristo alipomfufua kutoka kwa wafu
na kumweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa mbinguni
juu sana…” Waefeso 1:19-21
YESU ANAFANYA NINI SASA?
Yesu anatawala kama Mfalme juu ya mbingu na dunia yote.
Hii ina maana kwamba marais, mawaziri wakuu,
wafalme, madikteta na serikali zote hatimaye
zinawajibika kwake. Yeye ndiye Mfalme!
“…Yesu Kristo, shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza kutoka
kwa wafu, na mtawala wa wafalme wa dunia.”
Ufunuo 1:5
"...Mungu... sasa anawaamuru watu wote kila mahali kutubu,
kwa sababu ameweka siku ambayo atahukumu
ulimwengu kwa haki kupitia Mtu ambaye amemteua.
Amewapa watu wote uhakika wa jambo hili kwa kumfufua
kutoka kwa wafu." Matendo ya Mitume 17:30-31
"Yesu akaja na kusema nao, 'Nimepewa mamlaka yote
mbinguni na duniani.'"
Mathayo 28:18
Yesu anafanya kazi pamoja na wale wanaohubiri habari njema
za maisha yake, kifo, kuzikwa na kufufuka kwake.
Anafanya kazi pamoja nao kwa kutenda matendo makuu
ili kuthibitisha ukweli wa Neno lake.
"Nao wakatoka na kuhubiri kila mahali, Bwana
akifanya kazi pamoja nao na kulithibitisha neno kwa
ishara zilizofuatana nalo. Amina!" Marko 16:20
"Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,
mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la
Roho Mtakatifu, mkiwafundisha kuyashika mambo yote
niliyowaamuru; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote,
hata mwisho wa dahari. Amina." Mathayo 28:19-20
Yesu anamtuma Roho wake ili akae ndani ya wale wote
wanaomwamini na kumtii. Unaweza kumpokea
Roho Mtakatifu na kujazwa na uzima na nguvu Zake
leo!
“Tazama, nawaletea ahadi ya Baba yangu; lakini
kaeni katika mji wa Yerusalemu hata mtakapovikwa
nguvu kutoka juu.” Luka 24:49
“Naye alipokutana nao, aliwaagiza
wasiondoke Yerusalemu, bali
waingoje ahadi ya Baba, ‘ambayo,’ alisema, ‘mmeisikia
kwangu; kwa maana Yohana alibatiza kwa maji kweli,
lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya
siku chache…Lakini mtapokea NGUVU Roho Mtakatifu
atakapowajilia…” Matendo ya Mitume 1:4-5, 8
“Yeye [Yesu] Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume
kuwa Mkuu na Mwokozi, ili kutoa toba kwa Israeli na
msamaha wa dhambi. Nasi tu mashahidi wake kwa mambo
haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa
wale wanaomtii.” Matendo ya Mitume 5:31-32
Yesu anakaa mbinguni hadi mambo yote
yatakaporejeshwa na kuwekwa sawa kulingana na
kusudi la awali la Mungu.
“…ili Yeye [Mungu] amtume Yesu Kristo, ambaye
alihubiriwa kwenu hapo awali, ambaye mbingu lazima
zimpokee hadi nyakati za kurejeshwa kwa mambo yote,
ambayo Mungu ameyasema kwa kinywa cha manabii Wake
watakatifu tangu mwanzo wa ulimwengu.” Matendo ya Mitume 3:20-21
Yesu anangoja hadi maadui Wake wote
watakapofanywa kuwa kiti cha kuwekea miguu Yake. Adui wa mwisho
atakayeangamizwa ni mauti yenyewe. Mungu atakuwa na
watu wakamilifu duniani bila maadui waliosalia
kuangamizwa au kuleta madhara tena.
“Kwa maana lazima Yeye atawale hata atakapowaweka
maadui wote chini ya miguu Yake. Adui wa mwisho
atakayeangamizwa ni mauti.” 1 Wakorintho 15:25-26
“Lakini huyu, baada ya kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi
milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; tangu wakati huo
akingojea hata adui zake watakapofanywa kuwa kiti cha kuwekea miguu yake.”
Waebrania 10:12-13
“Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu wote mtakatifu,
maana dunia itajaa maarifa ya BWANA
[Mungu wa Milele, Yesu] kama maji yanavyoifunika bahari.”
Isaya 11:9

Maoni & Tafakari za Wasomaji (0)

Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!

Acha Tafakari Yako
NENO TIME
Sakinisha App ya NENO TIME
Upatikanaji wa haraka na masomo bila intaneti