ANNOUNCEMENT One Day International Apostolic Conference: Location: KIA (Mianzini) on 20th October 2026 Contact: 0692937637/0754757658
Kutubia matendo yasiyo na uhai.

Kutubia matendo yasiyo na uhai.

Text Size: 100%
PDF
Soma kwa Sauti:
Reading...

Kutubu ni nini?

1. Kutubu ni kugeuka ktk tabia zisizo faa, kuachana na Dhambi,  uasi, kutomtii MUNGU, Na kumgeukia MUNGU. 

MATENDO 3:19-20,

2. Kutubu inamaanisha: kubadilisha mawazo, nia mbaya, ikihusisha hisia ile hali ya  kuhisi majuto kwa sababu ya Dhambi mtu anazozitenda.

3. Dhambi hakika ni kupoteza mwelekeo na MUNGU, kuishi Maisha mabaya yenye kumchukiza MUNGU.

4. Tukitenda dhambi, ninani tunamkosea? Daudi anasema, Nimekutenda dhambi wewe peke yako.

ZABURI 51:4,

Ukitenda dhambi yoyote ile, Mfano. Uasherati, Usinzi, Ulevi. Usuda , usengenyaji,  Umbeya, Uongo. Nk, yote haya unamkosea MUNGU.

GALATIA 5:18-21,

1: Kila Mtu anatakiwa kutubu?

Kwa sababu wote wamefanya Dhambi, Na kupungukiwa na Utukufu wa MUNGU"

WARUMI 3:23, 

Mtume Paulo anasema, Basi, zamani zile za ujinga MUNGU alijifanya kama hazioni, bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu" 

MATENDO 17:30.

2: Kutubu ni mapenzi ya MUNGU kwa kila Mtu.

Tambua kwamba ni mapenzi ya MUNGU kila Mtu kutubu, 

= BWANA hakawii kuitimiza ahadi yake, Kama wengine wanavyokudhania kukawia, bali huvumilia kwenu, Maana hapendi Mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

2PETRO 3:9,

Je unakawia kuja kwa YESU kwa sababu ya mambo yasiyofaa unayoyafanya? Tafakari maana MUNGU anakusubiria utubu na kuacha na hayo. Na Je wewe uliyepata Neema ya Wokovu  kwa YESU, unamambo unayoyafanya kwa siri! Acha rudi kwenye mstari.

3: Watu wanapaswa kuhubiriwa ili watubu. 

YOHANA Mbatizaji alitengeneza njia kwa kuja kwake Masihi. 

Akasema, Tubuni; kwa Maana UFALME wa mbinguni umekaribia. 

MATHAYO 3:2,

YESU alianza huduma yake akihubiri toba. Tubuni; kwa Maana UFALME wa mbinguni umekaribia, MATHAYO 4:17,

Wanafunzi wa YESU nao walihubiri toba; 

Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. 

MARKO 6:12,

YESU aliwatuma wanafunzi wake wahubiri  ujumbe wa Toba kwa Mataifa yote.

Je, Ndugu umeshawahi kusikia NENO la MUNGU likihubiriwa! Na kama umesikia umedharau au umetafakari kile linachokuambia? Fikiri vizuri chukua hatua, Acha kuipenda dunia itakumaliza. 1YOHANA 2:15-17,

Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba KRISTO atatezwa na kufufuka siku ya tatu;

Na Kwamba Mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba, LUKA 24:46-47.

Siku ya pentecosti, PETRO alihubiri toba kama kama masharti ya kubatizwa na Kupokea ROHO Mtakatifu. 

Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO Mtakatifu. MATENDO 2:38.

SHALOM. Nitaendelea.

Maoni & Tafakari za Wasomaji (0)

Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!

Acha Tafakari Yako
NENO TIME
Sakinisha App ya NENO TIME
Upatikanaji wa haraka na masomo bila intaneti