NENO TIME — Anchored in Truth
Dhambi zinatudhuru kwa njia ipi?
1: Huzuni ya dunia - tunajiletea hukumu wenyewe kwa kuyatenda yasiyofaa ya dunia.
= mfano; huzuni ya dunia inakuja pale Mtu anapozini, akajikuta anaathiriwa na magonjwa mfano VVU (Ukimwi) n.k anaweza akajinyonga.
2: Huzuri ya MUNGU: Hii ni tunakubaliana na Dhambi zetu naye MUNGU anatusamehe.
1YOHANA 1:9,
Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya MUNGU hufanya toba liletalo Wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia huleta mauti, 2Korintho 7:10.
Toba inahusisha kuyabadilisha mawazo.
Toba inahusisha kubadilisha mawazo ambayo tunageuka kabisa kutoka kwa yale tumekuwa tukitenda na kugeukia yale ambayo MUNGU anataka tuyatende.
1. Mfano wa zakayo.
Zakayo alipompokea YESU, alibadilisha tabia zake za unyang 'anyi na akarudisha vitu vyote alivyokuwa ameiba na hata zaidi. LUKA 19:8,
2: Mwana mpotevu Luka 15:11-24, ni
Mfano wa mtu aliyepoteza mali alizopewa na baba yake, akazitumia kwa ukahaba.
Alitubu na akabadilika kabisa, (Aligeuka)
1: Alizingatia moyoni mwake; mstari 17, kutokana na huzuni ya dunia.
2: Akafanya maamzi bora mstari 18-19, toba ktk mawazo yake.
3: Alibadilika kulingana na mazimio ya ndani ya moyo wake. Mstari 20.
Je, Ndugu kunadhambi unaiona katika maisha yako? na hujui ni nini unapaswa kuja kwa YESU yeye ni wa Msamaha. ISAYA 1:18,
Kumbuka: Tambua haya masomo ni Msingi wa BIBLIA, yanaongea na kila mmoja, awe ameokoka, au hajaokoka, (Asante)
Somo hili nitalimalizia
Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!