NENO TIME — Anchored in Truth
Wakristo wanapaswa Kutubu.
Katika somo lililopita tulifika kipengele cha tatu.
Sasa tunaenda katika kipengele cha Nne.
4: Wakristo wanapaswa kutubu.
Soma 1YOHANA 1:8-10 , Tukisema Kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala Kweli haimo mwetu" mst 8. Tukisema Kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo wala NENO lake halimo mwetu" mstari 10.
Mstari 9 unatuambia jindo ya kufanya tukitenda dhambi, Tukakumbuka dhambi zetu, Yeye ni Mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Thahadhari hapa kwenye hii mistari, haikwambii uendelee kutenda dhambi kwa sababu kuna Toba,
Uliyepata Neema ya wokovu usiichezee: Kwa Maana Neema ya MUNGU iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa. Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, TITO 2:11-12,
Unapaswa kutambua tu wewe ni mwenye Dhambi, na ukitambua hilo basi unapaswa kuziungama Dhambi zako kwa YESU, Yeye ni Mwaminifu anaziondoa kabisa.
Tambua ukitubu umesamehewa dhambi zako kabisa wewe siyo mwenye dhambi tena. Wewe ni kiumbe kipya.
2KORINTHO 5:17, inasema: Kwa hiyo Kama Mtu akiwa ndani ya KRISTO, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, Tazama, yamekuwa Mapya.
5: Mtu asiyetii maagizo ya MUNGU ni Dhambi.
Dhambi inatutenga na MUNGU. Maana Mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa ktk NENO moja, amekosa juu ya yote. YAKOBO 2:10,
YESU anatufundisha kuhusu jambo ambalo linatoka ndani ya moyo wa mwanadamu, Na mambo hayo maovu yanamtia Mtu unajisi.
Soma. MARKO 7:21-23,
Aliyeokoka yeye siye mwenye dhambi, bali yeye ni Mtakatifu, ZABUR 16:3, Inasema; Kwa habari ya watakatifu walioko duniani,
Ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. ZABURI 30:4,
DANIEL 7:18. Inasema: Lakini watakatifu wa Yeye Aliye juu sana watapokea Ufalme na kuumiliki milele, naam, milele na milele, EBRANIA 12:28, EFESSO 1:1, 4. Wafilipi 1:1, Wakolosai 1:2, hii ni badhi inazungumzia watakatifu walioko duniani,
Mtu ye yote akikuambia hakuna Mtakatifu duniani, hata kama ni kiongozi wako wa dini mwambie wewe ni mwongo.
Kuna baadhi ya dini zimewambia watu ili uwe Mtakatifu mpaka ufe, huo ni uongo mtupu,
Usikubaliane na jambo linalohusina na MUNGU kama halina usibitisho wa BIBLIA.
SHALOM: nitaendelea na hili somo.
Hakuna maoni yaliyotumwa bado. Kuwa wa kwanza kutoa tafakari yako kuhusu somo hili!